MUSTAPHA Ghorbal, raia wa Algeria alionyesha kadi nne jana Aprili 9 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi kati ya Al Ahly na Simba.
Ni El-Shenawy kipa wa Al Ahly alionyeshwa kadi ya njano pekee huku tatu zote walionyeshwa wachezaji wa Simba wakati ubao ukisoma Al Ahly 1-0 Simba.
Ni Shomari Kapombe beki wa pembeni, Joash Onyango beki wa kati na kiraka Erasto Nyoni ambao walionyeshwa kadi hizo katika mchezo huo.
Nyoni alionekana akizungumza na mwamuzi huyo kwa hasira huku mshambuliaji namba moja Meddie Kagere naye alionekana akizungumza naye mara kwa mara na mwamuzi huyo raia wa Algeria.
Licha ya matokeo hayo Simba imetinga hatua ya robo fainali na inaongoza kundi A ikiwa na pointi 13 kibindoni huku Al Ahly ikiwa na pointi 11.
Kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea leo Aprili 10 kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.
Kumbuka mechi ya robo fainali ni simba na waaligeria pengine Refa alijichanganya kwa Erasto nyoni akidhani Thadeo Lwanga.Na kapombe akidhani.Morrisoni.
ReplyDelete