RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI. |
Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), limesema taarifa iliyoandikwa na Gazeti moja la
tarehe 15, Mei 2015 yenye kichwa cha habari “Nkurunziza ameweka picha mbaya
katika soka” haina uhusiano na TFF.
Katika
taarifa hiyo katibu wa chama cha makocha nchini (TAFCA), Michael Bundala
amenukuliwa akihusisha masuala ya mpira na hali ya kisiasa nchini Burundi.
TFF
imesikitishwa na kauli hii na inajitenga nayo. Kwa kua aliyetoa kauli hii ni
mwanafamilia ya mpira wa miguu nchini, uongozi wa TFF unafuatilia ili
kujua ni hatua gani zichukuliwe.
Jukumu la
TFF ni kuendeleza na kusimamia maendeleo ya mpira wa miguu na si
vinginevyo.
TFF
inawatakia wananchi wa Burundi hususani familia ya mpira, amani, utulivu na
baraka katika nchi yao.
0 COMMENTS:
Post a Comment