KOCHA Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solkjaer, anaamini kwamba namba ya leo ni ya bahati kwake anaweza kutwaa taji la Europa League mbele ya Villarreal inayonolewa na Kocha Mkuu, Unai Emery,
Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Villarreal kutinga hatua ya fainali ya Europa League katika historia na imebainsiha kwamba inahitaji pia kushinda taji hilo katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa saa 10:00 usiku Uwanja wa Gdansk huku ikitegemea uzoefu wa kocha wake Unai.
Solskjaer anaamini kwamba bahati yake ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya ndani ya Nou Camp, 1999 ikiwa imepita miaka 22 inaweza kujirudia kwa sababu alitwaa taji Mei 26 mbele ya Barcelona pia leo ni kumbukizi ya kuletwa duniani.
Ikiwa atafanikiwa kufanya hivyo kwa sasa atakuwa ni kocha wa kwanza kuipa taji la Europa League baada ya kupita miaka minne kwa kuwa mara ya mwisho United kunyanyua taji hilo ilikuwa ni mwaka 2017 wakati wa Kocha Mkuu, Jose Mourinho.
Ila kwa sasa Solskjaer anaamini kwamba ni muda wa ushindi kwake na vijana wake watampa mafanikio jambo ambalo litakuwa ni kufungua milango iliyokuwa imefungwa.
"Huu ni usiku mkubwa wetu. Lazima tufanye kitu kwa ajili ya fainali ili tupate taji kwani hilo ni jambo la muhimu kwetu. Wachezaji wakipata ladha ya ushindi na kushinda taji tutakwenda nao kwa kasi hasa miaka ijayo katika ari ya upambanaji. Tutafanya sasa na tutapumzika.
"Ninawaamini wachezaji wangu na ninaona jambo linatokea kwao zaidi ya zaidi ni kujiamini na kujitoa kwa ajili ya kupata ushindi. Kumaliza katika katika nafasi ya pili ni jambo nzuri,"
0 COMMENTS:
Post a Comment