NYOTA wa Tanzania Prisons, Salum Kimenya amesema kuwa ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu huu wa 2020/21 umezidi kuwa mkubwa tofauti na msimu uliopita huku mechi zao mbele ya Simba na Yanga zikiwa na ushindani wa kipekee.
Katika mabao 23 ambayo yamefungwa Kimenya alifunga bao moja licha ya kwamba ni beki na alimtungua kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula kwa pigo huru.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kimenya amesema kuwa kila mechi ambayo wanacheza kwa sasa inakuwa ni sawa na fainali kwa kuwa kila timu inahitaji pointi tatu.
"Kwa sasa msimu huu ni mgumu na kila timu inahitaji pointi tatu hivyo jambo hilo linatufanya nasi tuzidi kupambana kwenye kila mchezo ambao tunacheza.
"Nakumbuka kwamba kwenye mechi zetu mbili ambazo tulicheza na Yanga na Simba haikuwa kazi nyepesi kukamilisha dk 90 hasa ukizingatia kwamba ni timu kubwa na zina wachezaji wenye kujituma jambo ambalo linafanya ushindani kuwa wa kipekee" amesema.
Prisons ipo nafasi ya 8 ina pointi 42 baada ya kucheza jumla ya mechi 32 ndani ya Ligi Kuu Bara.
Ukimfunga kipa bora unapata sifa na inakuwa ndo utambulisho wako. Mfunge kipa wa Utopolo kama utapata sifa yoyote
ReplyDelete