DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kwa mwendo ambao wanakwenda nao kwa sasa bado hajafikiria kwamba kuna timu inaweza kuwafunga katika mechi za ushindani kutokana na uwezo wa wachezaji wake.
Kwenye ligi, Simba ipo nafasi ya kwanza na ina pointi 73 baada ya kucheza mechi 29 mchezo wake ujao kwenye ligi ni dhidi ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa Mkapa Julai 3.
Akizungumza na Saleh Jembe, Gomes amesema kuwa kwenye soka jambo lolote linaweza kutokea ila anaamini kwamba vijana wake wapo imara.
"Sijafikiria kwamba kama kuna timu ambayo inaweza kutufunga ingawa kwenye mpira jambo lolote linaweza kutokea.
"Bado tuna nafasi ya kufanya vizuri na wachezaji wangu ninawaamini katika yale ambayo wanafanya hivyo tutazidi kupambana ili kuwa imara wakati wote," amesema.
Gomes amekiongoza kikosi cha Simba kutinga hatua ya Kombe la Fainali kwenye Kombe la Shirikisho na inatarajia kukutana na Yanga, Julai 25, Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
0 COMMENTS:
Post a Comment