June 29, 2021

 

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amefunguka kuwa siri kubwa ya ubora kikosi chake katika kuchezea mpira inatokana na balansi inayoletwa na matumizi ya viungo wawili wakabaji, kulinganisha na wanapotumia kiungo mmoja pekee.

Ndani ya kikosi cha Simba, Gomes amekuwa akiwatumia zaidi Taddeo Lwanga na Mzamiru Yassin kama pacha ya viungo wakabaji ndani ya kikosi chake katika michezo mingi, hali inayowapa urahisi viungo wa juu wa Simba kuwa na wakati mzuri wa kuchezea mpira.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Gomes alisema: “Tumekuwa tukitumia mifumo mbalimbali kuendana na wapinzani ambao tunakutana nao, lakini naweza kusema kikosi chetu kinakuwa na balansi kubwa na kucheza vizuri zaidi iwapo tunacheza na viungo wawili wakabaji.


“Lakini kuna wakati tunalazimika kujitoa mhanga kwa kutumia kiungo mmoja pekee hasa tunapotumia mfumo wa 3-5-2, kama ambavyo tulicheza dhidi ya Mbeya City," .


Mchezo ujao wa Simba ni dhidi ya Yanga unatarajiwa kuchezwa Julai 3, Uwanja wa Mkapa saa 11:00 jioni.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic