June 29, 2021

 


ZIKIWA zimebeki siku nne kwa watani wa jadi, Simba na Yanga kukutana Uwanja wa Mkapa, rekodi zinaonyesha kuwa makocha wawili Didier Gomes wa Simba na Nassredine Nabi wa Yanga walikuwa na kazi ya kukimbizana ndani ya dk 450.

Kwenye mechi zao tano za hivi karibuni kwenye ligi Gomes alionekana kumkimbiza Nabi kwa kusepa na pointi nyingi ambazo ni 15 huku Nabi akisepa na pointi zake 10.

Ni Gomes raia wa Ufaransa alishinda mechi zake 5 alizokaa kwenye benchi na alishuhudia jumla ya mabao 14 wachezaji wake wakifunga na mabao matatu waliokota kwenye nyavu zao.

Ndani ya dakika 450 msako wa pointi 15 Simba ilisepa na pointi zote mazima ambapo ugenini ilikuwa kwenye mechi tatu na nyumbani ilikuwa kwenye mechi mbili.

Mwendo wa Gomes ulikuwa namna hii:-Aprili 27, Simba 3-1 Dodoma Jiji,Uwanja wa Mkapa, Mei 29, Namungo 1-3 Simba,Uwanja wa Majaliwa, Juni 3, Ruvu Shooting 0-3 Simba, uwanja wa CCM Kirumba, Juni 19, Polisi Tanzania 0-1 Simba, Uwanja wa CCM Kirumba, Juni 22, Simba 4-1 Mbeya City, Uwanja wa Mkapa.

Kwa upande wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi katika mechi tano ambazo ni dk 450, Yanga ilipoteza mchezo mmoja, sare moja na ushindi katika mechi tatu.

Ilikuwa msako wa pointi 15, Nabi alisepa na pointi 10 na kuyeyusha pointi tano mazima huku wachezaji wake wakifunga jumla ya mabao 8 na kufungwa mabao matano.

Mwendo wake ulikuwa namna hii:-Aprili 25, Yanga 0-1 Azam FC, Uwanja wa Mkapa, Mei 15, Namungo 0-0 Yanga, Uwanja wa Majaliwa, Mei 19, JKT Tanzania 0-2 Yanga, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, Juni 17, Ruvu Shooting 2-3 Yanga, Uwanja wa Mkapa, Juni 20, Yanga 3-2 Mwadui FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic