MWENYEKITI wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu ameweka wazi kuwa Uongozi wa klabu hiyo unajivunia kuwa sehemu ya ushirikishwaji katika mchakato wa kuanza kwa michuano mikubwa ya African Super League.
Michuano hiyo ambayo mwanzo
ilitokana na pendekezo la Rais wa Shirikisho la soka duniani, Gian Infantino
ambaye alipendekeza kuanzishwa kwa ligi hiyo itakayokuwa na timu 20 za kudumu,
huku pia kukiwa na timu ambazo zitakuwa zikipambana kusaka nafasi ya kucheza
michuano hiyo.
Rais wa Shirikisho la Soka Afrika, Patrice Motsepe hivi karibuni amesema: “Wamejifunza mengi kuhusu jaribio la Super League ya Ulaya ambalo lilifeli, na ana matumaini makubwa kuwa, kutokana na kujifunza huko watafanikiwa katika mpango wa African Super League.
Akizungumzia kuhusu mpango huo, Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amesema: “Kuhusiana na michuano ya Super League, ni ngumu kuzungumza kitu kwa sasa kwa kuwa tupo katika hatua za awali za mazungumzo juu ya hilo.
“Kwa sasa hatuwezi kusema
tumefikia katika hatua gani kwa kuwa kama ambavyo nimesema tupo katika hatua za
awali, na tutatoa taarifa zaidi pale mchakato utakapokamilika, lakini kama
uongozi wa Simba tunajivunia kuwa sehemu ya mchakato huu, hii bila shaka
inaonyesha ukubwa ambao kama timu tunao.”
0 COMMENTS:
Post a Comment