August 23, 2021

 JINA lake halikupewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye ardhi ya Tanzania ila alifanikiwa kuwaonyesha wengi maana halisi ya kile ambacho alikuwa nacho kwenye miguu yake.


Anaitwa Yacouba Songne,  mshambuliaji namba moja wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia. 


Jezi yake anayopenda kuitumia ni namba 10 mgongoni ambayo inamtambulisha kwa mashabiki zake na washakji zake wa Yanga ambao wapo naye bega kwa bega.



Anakumbukwa kwa bao lake muhimu mbele ya Tanzania Prisons,  Uwanja wa Nelson Mandela katila mchezo wa Kombe la Shirikisho ambapo alifunga bao hilo kwa pasi ya Said Ntibanzokiza. 


Ukiweka kando hilo pia ni nyota ambaye anashikilia rekodi ya kuhusika katika mabao mengi ndani ya Yanga katika mchezo mmoja ilikuwa mbele ya Mwadui FC.


Wakati ubao wa Uwanja wa Kambarage ukisoma Mwadui FC 0-5 Yanga yeye alipachika mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao na kumfanya ahusike katika mabao manne ndani ya mchezo mmoja.


Kibindoni katika ligi ana mabao 8 na pasi tano za mabao hivyo amehusika katika mabao 13 ndani ya Yanga kati ya mabao 52 yaliyofungwa msimu wa 2020/21.


Bao lake la kwanza alifunga Uwanja wa Mkapa ilikuwa mbele ya Coastal Union zama za Zlatko Krmpotic ambaye ulikuwa ni mchezo wake wa wa mwisho kwa kuwa baada ya mchezo huo kukamilika alichimbishwa mazima na nafasi yake ikachukuliwa na Cedric Kaze ambaye naye hakudumu Yanga na sasa ni zama za Nabi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic