August 12, 2021


 UONGOZI wa Klabu ya KMC iliyomaliza ligi ikiwa nafasi ya tano na pointi 48 baada ya kucheza mechi 34 umebainisha kwamba utakamilisha usajili wa majembe ya kazi utakapopata ripoti.


Dirisha la usajili likiwa limefunguliwa tayari timu zimeanza kuingia sokoni kusaka nyota wapya ambao watafanya kazi na timu zao ila kwa KMC wao bado hawajaanza vurugu zao.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC wazee wa pira kodi, Christina Mwagala amesema kuwa wanatambua ni wakati wa usajili lakini watafanya kazi pale watakapopokea ripoti.


“Kwa sasa tupo na tunaendelea kufanya kazi imekuwa ni kawaida yetu kila wakati wa usajili kuwa kimya bila vurugu lakini mwisho wa siku tunafanya usajili mzuri.


"Kinachosubiriwa wakati huu ni ripoti ya mwalimu, hatuwezi kusajili bila kutumia ripoti ambayo kwa sasa bado hatujakabidhiwa ikiwa tayari kila kitu kitafanyika,” amesema Christina.



2 COMMENTS:

  1. Semeni ukweli, mnasubiria watakao temwa Simba na Yanga

    ReplyDelete
  2. Au mambo ya fedha mgogoro msifiche semen wampe wachezaji wa mkopo simba tutampa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic