August 6, 2021


 KOCHA Msaidizi wa AS Vita, Raoul Shungu ameibuka na kusema kuwa kitendo cha Yanga kuwanasa nyota wake wawili, mshambuliaji Fiston Mayele na beki Djuma Shaban basi ana uhakika wapinzani wao wakiwemo Simba watapata tabu kutokana na kuutambua ubora wa wachezaji hao.


Shungu ametoa kauli hiyo baada ya 
Yanga kumalizana na nyota hao wa AS Vita kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Shungu alisema kuwa kwake Mayele na Djuma ni wachezaji wakubwa na wenye uzoefu wa michuano mikubwa, hivyo anaamini watakuwa na mchango wa kutosha ndani ya Yanga katika msimu ujao wa ligi.

 

“Kiukweli sina shida ya ubora wa Djuma wala Mayele kwa sababu ni wachezaji wenye uzoefu mkubwa na michuano ya kimataifa na wana uwezo wa kucheza kwenye uwanja wowote kama ilivyokuwa kwa Mukoko (Tonombe) na Tuisila (Kisinda) ambavyo wamefanikiwa katika ligi ya huko.

 

"Naamini timu pinzani watapata tabu kutokana na namna Yanga walivyoamua kuijenga timu yao kwa sababu wanataka kuwa bora, wanataka kushinda makombe kama ilivyo kuwa huko nyuma na aina ya wachezaji wanaojaribu kuwaleta wakiwemo Mayele na Djuma,” alisema Shungu.

9 COMMENTS:

  1. Kwa simba hii Yanga asitegemee maajabu na hao wachezaji wake wapya. Simba ana timu tayari, Yanga ana wachezaji itategemea muda gani itawachukua ili kuwa na timu.

    ReplyDelete
  2. mjomba hapa ni bongo sio congo,kama huyo djuma shaban anaweza asicheze mpira kabisa,wako wapi akina fiston,akin sapong ambao ni top score wa kwao leo hii kashindwa ligi karudi kwao,acha wewe ngoja uone.

    ReplyDelete
  3. Wacongo wanapigiana debe kuja kuvuna pesa ya wabongo, hilo halina jipya.

    ReplyDelete
  4. Mikia tulieni, waliopo wanawatoa jasho je maingizo haya ya viwango?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ahhhgh. Tunotolewa jasho ni sisi sio mikia. Angalia mpira wetu. Mifaulo na piga mbele bahatisha. Tujitizame Kagame. Timu za ovyo zinatudhinda. Tatizo mbeleko za marefa hatupati. Kina Manara wanaotufanyia hujuma wameshtukiwa. Sasa ndio tutabaki lia lia. Angalieni sana mwaka huu najua ni kufedheheka kwenda mbele. Na kama hamjui hata huyo kocha wetu ni garasa tu...

      Delete
  5. Utopolo hawana jipya wanatafutiana kula tu labda waje kwenye mziki sio mpira wachezaji wa maana watawapata yanga

    ReplyDelete
  6. Mikia wanapenda kutoa mifano hasi ili kujipa moyo, mbona hawasemi TK master wala mukoko?

    ReplyDelete
  7. Mukoko mpiganaji mieleka. Boko mwanasoka bora. Magoli yake sawa na yanga nzima ya mukoko na tuisila

    ReplyDelete
  8. Shida Mikia wote akili zenu Ni mbumbumbu kumbuka Rage aliwaita na uthibitisho Ni Haji Manara leo ,kipupwe kimemrudisha utu mnamtukana lkn siku zote mnamwita shujaha,bila kusahau MO naye kawandondosha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic