WAKATI ikielezwa kuwa tayari Kibu Dennis amemalizana na Simba kwa ajili ya msimu ujao uongozi wa timu hiyo umeweka wazi kwamba kwa sasa upo chimbo kusaka wachezaji wapya.
Imeelezwa kuwa kwa sasa Kibu yupo Dar kwa lengo la kumalizana na
mabingwa wa Tanzania Simba ambao walimpeke ghym kujiweka fiti.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Kocha Msaidizi wa Mbeya City,
Mathias Rwambiza alisema kuwa hesabu kubwa ni kusajili wachezaji wazuri ili
kuziba nafasi kwa ajili ya wale ambao wataondoka.
“Ikiwa kuna mchezaji ataondoka basi tutafanya kazi kubwa ya
kuweza kumtafuta mbadala wake kwa kuwa hatuwezi kuwazuia wachezaji wetu ambao
watahitajika na timu nyingine haitupi tabu.
“Wale watakaoondoka basi kazi itakuwa ni kumtafuta mbadala wake
kikubwa ni kuona kwamba timu haiypi wala kupoteza ramani,” alisema.








0 COMMENTS:
Post a Comment