August 21, 2021


 BAADA ya tetesi kueleza kuwa kiungo aliyekuwa mali ya Simba msimu wa 2020/21 Luis Miquissone kwamba ataibukia kwa watani zao wa jadi Yanga, uongozi wa timu ya Simba umesema kuwa suala hilo halipo kwa wakati huu.

Luis msimu ujao wa 2021/22 hatakuwa mali ya Simba baada ya uongozi wa timu hiyo kubainisha kwamba hatakuwa ndani ya kikosi hicho kwa wakati ujao na hawajaweka wazi timu ambayo atakuwepo msimu ujao.

Habari zinaeleza kuwa Luis atakuwa ni mali ya Al Ahly ya Misri na uvumi ukaeleza kwamba atatambulishwa Yanga siku ya Mwananchi, Agosti 29, Uwanja wa Mkapa.

Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema kuwa wengi wanasema mambo ambayo hayapo na hivyo hakuna jambo hilo.

"Wengi wanasema kwamba kwa sasa Luis atakwenda Yanga, jambo hilo sio kweli kwani mchezaji huyo amepata timu nje na sio huko anakotajwa kwenda," .

26 COMMENTS:


  1. Masikimi Matopolo ndoto zao zinawatesa vibaya tena wala hawana haya

    ReplyDelete
  2. Hawa wamekalia uvumi tu, Simba iliishaondoka huko, subiri wao waendeleze libeneke la Wakongoman

    ReplyDelete
    Replies
    1. Si kweli kwamba Simba ilishatoka huko, maana bado inaendelea na kamchezo ka kusainisha wachezaji wenye mkataba,tena ni aibu kugombania mchezaji hata na timu ndogo kama Kagera Sugar.

      Delete
    2. N kwel kabsa, Yan Wanatia aibu Kwa kwel.

      Delete
  3. Achani kukurupuka kwani yanga wamemtambulisha inawezekana hamna la kufanya ndo maana mnacoment kila kitu

    ReplyDelete
  4. Jaman Luis ameuzwa au amevunja mkataba ma'am hajulikan alikoend

    ReplyDelete
  5. Saleh jembe huna wandishi kaka wanakutilisha aibu

    ReplyDelete
  6. Ht triple c na picha ilitumwa ya kwamba amekuwa alizeti!

    ReplyDelete
  7. Simba wametengeneza tu hii ishu ili waje wakanushe pia. Sijui wanapataga umaarufu gani?

    ReplyDelete
  8. Luis sio wa Simba na hajatambulishwa kwa nini kuhamgaika kutolea ufafanuzi? Acheni kuweweseka

    ReplyDelete
  9. Mnateseka na nini mikia fc wakati miqueson hawahusu kwasasa

    ReplyDelete
  10. Huko Moroco Simba 1 Wapinzani 1 bao la Simba Morrison

    ReplyDelete
  11. Yanga wanauwezo wa kumchukua.coz ni timu bora2 amin

    ReplyDelete
  12. Cmba nitim kubwa kwann hawatuweki was jaman

    ReplyDelete
  13. Mm ni Yanga lakini nimeona kavalishwa jezi yetu. Na Senzo ndiye anamsemea kuwa alimleta Simba na sasa anamrudisha kwa Wananchi. Ngoja tuone siku yetu pale kwa mkapa

    ReplyDelete
  14. Ah wote mizinguo tu syo simba wala yanga wrote hawaelewek

    ReplyDelete
  15. Tatizo ni huyu salehe jembe cjui ana waandishi gan yaaan source zake hta hazielewk

    ReplyDelete
  16. Mautopolo yamesajili lakini tamaa yao kubwa kusikia luis katua kwao

    ReplyDelete
  17. Mbona mnaweweseka mikia tulizeni mshono luis kaondoka na hamjui alipo enda sasa subirieni atakapo tambulishwa... Kwan Yanga wai wamemtambulisha...?! Fanya kuleta habari za uhakika usilete tetesi unakuwa mtoa tarifa pasipo kuwa m uhakika... Au moo kakutuma kwa kuwa anakulipa mshahara🤣

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic