BAADA ya kukamilisha usajili wa kujiunga na Simba, aliyekuwa mshambuliaji wa Mbeya City, Kibu Denis, ameanza programu maalum ya mazoezi ya gym kwa ajili ya kujiweka sawa kuelekea msimu ujao wa 2021/22.
Inaelezwa kuwa, tayari Kibu amekamilisha kila kitu na Simba kwa ajili ya kuwatumikia msimu ujao, na sasa anasubiri kutambulishwa rasmi kama ambavyo wachezaji wengine wapya wa kikosi hicho walivyofanyiwa.
Kibu amesajiliwa Simba kama pendekezo la Kocha Mkuu, Didier Gomes ambapo anakuja kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo, ambayo inatajwa iko kwenye mpango wa kuachana na straika mmoja.
Akiwa na Mbeya City msimu uliopita, Kibu alionesha uwezo alifunga mabao sita na kupata nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi, Juni, mwaka huu.
Kuhusu usajili wake, Kibu aliliambia Spoti Xtra kwamba: “Nipo Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha usajili wangu kwenye klabu moja kubwa, tuendelee kusubiri kila kitu kitawekwa wazi," .








Huyo Bwawa Mdogo anaonekana yupo vizuri akizingatia nidhamu ya kazi atatoka. Simba kuna ugumu fulani kwa wachezaji wazawa hasa vijana kutoboa lakini tuwakumbushe vijana kuwa akina samata walitokea hapo hapo.Mpira wa Sasa unachezwa kwa Kasi zaidi na kujituma zaidi kuendana na mahitaji ya Mwalimu lakini tatizo kubwa la watanzania na si kwa wachezaji mpira tu hata kwenye sekta nyengine ni kwamba kujisimamia wenyewe kwa nidhamu ile ile ya kanuni ya majukumu husika hatuwezi mpaka tusukumwe Sasa kwa bahati mbaya Sana kwenye mpira hawa walimu wetu wa kigeni huwa hawanaga muda huo wa kumpushi mchezaji kugombaniwa namba na mchezaji mwenyewe ni wajibu wako wewe mwenyewe mchezaji kujituma na Mualimu akuamimi. Mpira ni mchezo wa wazi ukipata nafasi mtibitishie Mwalimu. Ukiona bado hakuamini basi bado Kuna kazi ya ziada unatakiwa kufanya ili kukabalika hakuna figisu Wala ujanja ujanja kwenye kazi ya mpira au tunguli. Tunguli zitakuja kukuzingua kwani tatizo sio kupata namba tatizo ni kutimiza majukumu yako ipasavyo uwanjani.Vijana wanapaswa kujifunza haya mambo la sivyo tutalaumu simba inaua vipaji kumbe vipaji vinaiua simba kwani kipaji bila ya kujituma ni sawa na BMW isiokuwa na mafuta.
ReplyDeleteKweli kabxa mjumbe!
ReplyDeleteKama wanaocomment humu wengi msingekuwa bias ingependeza,kwangu nakubaliana na hiyo unayosema lkn Kumbuka Kuna Ilanfya,Mhilu,Bocco,Mugalu nadhani na Kagere na vilevile Kumbuka Kocha huyo anapenda Sana kuchezesha wawili au mmoja so ukweli ajitambue ,ILa sikuoana ulazima wa Simba kuwa na mastriker wengi hv kumbuka Adam Salamba naye.
ReplyDeleteKifupi kavutiwa na mkwanja ninacho weza kuamini cse amesajiliwa Kocha akiwepo inawezekena Ana mpango naye.
ReplyDelete