KESHO Agosti 7 ni siku ya uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) ambao unatarajiwa kufanyika jijini Tanga.
Tayari wajumbe wote wameshawasili Tanga kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa uchaguzi ambao ulikuwa unasubiriwa kwa shauku.
Ni nafasi ya Urais ambapo Wallace Karia anatarajiwa kuthibitishwa na wajumbe kwa sababu jina lake lilipita peke yake kwenye mchujo.
Wajumbe ni 17 ambao wanawania nafasi kwenye uongozi TFF.
Kwa mujibu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Shirikisho
la Soka Tanzania, (TFF) Wakili Kiomoni Kibamba amesema kuwa kila kitu kipo sawa
kwa ajili ya uchaguzi.








Karia mikumi tena
ReplyDelete