August 11, 2021


 WAZIR Junior, nyota wa kikosi cha Yanga amesema kuwa hesabu zake kwa msimu ujao wa 2021/22 ni kuwa mfungaji bora ndani ya kikosi hicho.

Junior ni ingizo jipya ndani ya Yanga aliibuka hapo akitokea kikosi cha Mbao FC hajawa na nafasi kikosi cha kwanza jambo ambalo limemfanya akwame kufunga mabao zaidi ya matano.

Kibindoni amemaliza akiwa na mabao mawili kwenye ligi pia kwenye Kombe la Kagame alitupia bao moja katika mechi tatu alizocheza na Yanga iliishia hatua ya makundi.

Nyota huyo amesema:"Kwa msimu ujao malengo yangu ni kuwa mfungaji bora na hili linawezekana, wakati huu ilikuwa ngumu kutokana na ushindani wa namba.

"Kuhusu nafasi hilo lipo chini ya mwalimu hivyo nikipata nafasi wakati wa msimu ujao nitapambana ili kufanya vizuri na hilo inawezekana," amesema Junior.

Kikosi cha Yanga kinatarajia kukwea pipa kuelekea nchini Morocco  kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22.

Kilimaliza ligi kikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na kinara wa utupiaji alikuwa ni Yacouba Songne ambaye alitupia mabao nane.

5 COMMENTS:

  1. Kila la heri kwake...japo kazi yake ya kwanza ni kuhakikisha anapata nafasi kwenye kikosi ndipo apiganie kuwa mfungaji bora!

    ReplyDelete
  2. Kwa kiwango alichoonyesha ktk ligi ni dhahiri hawezi kuwa mfungaji bora

    ReplyDelete
  3. Angetolewa kwa mkopo ili apate nafasi ya ku improve lkn kikosi cha kwanza kwa Yanga hii itakua ngumu, hata washabiki watamchoka mapema

    ReplyDelete
  4. Jee hesabu zako zilikujibu nini, ni utakuwa bora kuliko Bocco na Kagere Kwa kufunga hivo vigoli vitatu au vine

    ReplyDelete
  5. Ufungaji bora kwenye ligii gani amechemka kagame ataweza ligii ya wanaume asitudanganye labda kwenye ndondoo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic