UONGOZI wa klabu ya Yanga umeweka
wazi kuwa upo katika mazungumzo ya kuwaongeza mikataba kocha msaidi wa timu
hiyo, kocha wa viungo na daktari wa misuli mara baada ya mikataba yao ya awali
kutamatika ndani ya Yanga.
Kocha Msaidizi, Sghir Hammadi
mwenye uraia wa Tunisia, kocha wa viungo Mmorocco, Jawab Sabri na Mchua misuli wa
Yanga mwenye uraia wa Afrika
Kusini, Fareed Cassiem wote hawapo katika kambi ya Yanga iliyopo nchini Morocco.
Yanga kwa sasa ipo nchini Morocco
ambapo klabu hiyo imeweka kambi maalumu ya siku 10 kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, wa michuano
mbalimbali ambayo Yanga itashiriki katika msimu ujao.
Chanzo cha ndani kutoka Yanga
kimetuambia kuwa makocha hao wote watatu wamemaliza mikataba
yao, huku wengine wakiwa wapo katika mazungumzo na timu nyingine japo klabu ya
Yanga wapo katika mazungumzo ya kuwaongezea mikataba mipya.
“Ni kweli makocha hao wote mikataba yao
imetamatika ndani ya Yanga, na wapo ambao walikuwa kwenye mazungumzo ya kujiunga
na klabu zingine huku Yanga nao wakifanya nao mazungumzo ya kuhitaji
kuwaongezea mikataba mipya.
Akizungumzia sakata hilo Ofisa habari wa Yanga Hassani Bumbuli amesema: “Mikataba ya makocha hao
imemalizika hivyo kama klabu tupo katika mipango ya kuwaongezea mikataba mipya
hivyo wanaweza wakaonekana msimu ujao, au wasionekane,” Amesema kiongozi huyo.







Ingekuwa Simba vingetengenezwa vipindi maalum kwanini wasiwaongezee mikataba kabla. Kwa Utopolo kimyaa. Hizi njama za wachambuzi uchwara hazitawafikisha popote.
ReplyDeleteSijui mnawaza kwa kupitia makalio mashabiki wa mikia? Umewahi kuona kipindi Maalum cha kuzungumzia makocha wasaidizi wa timu yenu?
DeleteWaandishi uchwara wote kimyaaa. Wako bize kuokoteza uzushi kuhusu simba. Andikeni hayo sasa
ReplyDeleteHahahaha upuuzi na ushuzi tu ndo umeandikwa hapo, et chanzo cha kuaminika! Nyie mko hapa bongo timu iko morroco arafu hata chanzo hujaweka unasema et chanzo cha kuaminika! Nguruwe fc wewe
ReplyDeleteKwahiyo hata hapo gazeti la salehjembe mtu akimaliza mkataba wake wa kazi unataka uandike stori ya kuleta mjadala? Mbona ni kitu cha kawaida ambacho hakihitaji mjadala
ReplyDeleteHuenda ikawa chao hawajapokea
ReplyDeleteNini yanga faida waliopata kutokana na kambi yao Morocco. Mimi nahisi walikwenda kutembea na kurudi nyumbani na kulalamika joto kali wakimuacha Myama aendelee na kile na kile walichokudia nacho. Kwanza waliisifu hali ya hewa na kusema ni kama ile ya nhumbani. Si bure
ReplyDeleteKichwa Cha habar na maelezo haviendani kabisaa so wandish mnazingua Sana na maelezo yenu.
ReplyDeleteNikishaona mwandishi ni salehe jembe si a haha ya kusoma kilichoandikwa na jua ni pumba tupu
ReplyDelete