CEDRIC Kaze aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga msimu wa 2020/21 kabla ya kuchimbishwa lwa kile kilichoelezwa kuwa mwendo mbovu wa timu na kutokwenda sawa na falsafa ya timu hiyo ametua Bongo usiku wa kuamkia leo.
Inaelezwa kuwa ametua kwa ajili ya kumalizana na mabosi wake wa zamani Yanga ambao wanahitaji huduma yake.
Anatarajiwa kuwa kwenye benchi la ufundi akiwa ni kocha msaidizi akishirikiana na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia.
Kabla ya kusepa baada ya kuchukua mikoba ya Zlatko Krmpotic, Kaze aliwapa Yanga taji la Mapinduzi baada ya kushinda kwenye fainali mbele ya Simba.
Sasa benchi la ufundi la Yanga litakuwa na Kaze pamoja na Nabi kuelekea kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi, Septemba 25, Uwanja wa Mkapa watakapomenyana na Simba katika Ngao ya Jamii.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga, Dominick Albinius amesema kuwa watatoa majibu leo kuhusu kumpa mkataba.
Jamaa wanaweweseka
ReplyDeleteKwakweli Yanga wanateseka aisee. Inabidi wafuate Ushauri wa Magoma la sivyo Bundi ataendelea kuinyea Yanga.
DeleteSasa viongozi wetu mmeanza kuzingua sanaaa
ReplyDeleteHiyo JEURI YA YANGA YA KUTIMUA NA KUREJESHA ITAKUJA KUWAGHARIMU KWASABABU HAKUNA MWANADAMU ANAYEPENDA KUTIMULIWA AKABAKI BILA KINYONGO NA HASIRA ZA KUTIMULIWA !
ReplyDeleteKUNA SIKU ATAKUJA KUUZA MECHI ILI KULIPA KISASI!
Makolo fc tulieni hivo hivo
ReplyDeleteUkiskia mama j fc aka utopolo ndio huu sasa mlimfukuza kwa7bu gan na mmemrudsha kwa7bu gan
ReplyDeleteSasa hii siku moja iliyobaki ndio atatengeneza timu? Hebu Yanga acheni kutafuta sababu za kulaumu makocha.
ReplyDeleteIle methali unaikumbuka?,siku ya kufa nyani, miti yote huteleza
ReplyDeleteKuna mtu juzi kaandika kuwa Yanga kutolewa mapema CAF Champions League ni kichefuchefu.Naona na nyinyi mmepata kichefuchefu Kaze kurudi.Mkapime MIMBA clinic na waliowapa ujauzito kwani kichefuchefu ndio hali ya mjamzito.Clinic ni miezi yote mpaka mkijifungua
ReplyDelete