September 22, 2021

 


KOCHA Mkuu wa Azam FC, George Lwandamina, baada ya kufanikisha timu hiyo kuvuka hatua ya awali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika,tayari amerudisha kambini jeshi lake kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22.

 

Azam imefanikiwa kuiondosha Horseed ya Somalia kwa jumla ya mabao 4-1 katika mchezo wa hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo sasa inakwenda kucheza dhidi ya Pyramid ya Misri.

 

Akizungumza na Spoti XtraOfisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ alisema: “Timu baada ya kumaliza mechi ya kimataifa ilipata mapumziko ila imerudi kambini kwa ajili ya maandalizi ya ligi na mashindano mengine.

 

“Majeruhi waliopo kwenye kikosi ni wawili tu ambao ni Prince Dube ambaye alifanyiwa upasuaji hivi karibuni na Charles Zulu, ila wengine wote wapo vizuri.”


Mchezo wa kwanza kwa Azam FC kwenye ufunguzi wa ligi ni dhidi ya Coastal Union na unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic