September 17, 2021


 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba mchezo wao wa marudio dhidi ya Rivers United hautakuwa mwepesi ila wamejipanga kuweza kufanya vizuri.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Rivers United kwenye mchezo wa marudio.

Mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unatarajiwa kuchezwa nchini Nigeria Septemba 19.

Katika ule mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 0-1 Yanga hivyo kazi kubwa ipo kwenye kupindua matokeo ugenini.

Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amesema:"Tunajua mechi za ugenini zina visa na mikasa mingi, tumejipanga na tumejiandaa na hilo na ndiyo maana tulituma watu imara wakufanya maandalizi yote kabla ya timu kufika.


"Tunaenda kucheza mechi ambayo kwa vyovyote vile itakuwa ngumu, mechi za ugenini kwenye ligi ya mabingwa siku zote huwa ni ngumu na hilo jambo tunalitarajia," .

Ni Senzo Mbatha ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Yanga kwa muda aliweza kutangulia nchini Nigeria na kwa sasa yupo huko akisubiri kuwapokea Yanga.

Mbatha ameweka wazi kuwa kila kitu kinakwenda sawa licha ya changamoto za soka la Afrika ambazo huwa hazikosekani.

6 COMMENTS:

  1. Yaani yanga kweli hawatumii akili, mnamtanguliza senzo? Of all the people hadi kumwamini senzo? Huyo jamaaanaenda kupiga dili anawauza mchana kweupe, anauchungu gani na yanga au soka la Tanzania kwa ujumla?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Je wewe na yule kijana wa utopolo mmeisaidia nini Yanga zaidi ya majungu na kutaka muonekane??

      Delete
  2. Mmmh! Some people still trust Senzo! Let us be serious guys.,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tanzanians!!! Wenzetu hawawazi kama tuwazavyo sisi. Sisi hatujali ajira zetu wenzetu wanajua maana ya ajira zao ndio maana wanaheshimika huku sisi midomo ndio mikubwa na hatuthaminiki

      Delete
    2. Bora Senzo kuliko hawa akina Haji au Mwakalebela. Huyu ana ujira Yanga, hao wengine wapo pale kwa kudra za mwenyezi Mungu.

      Delete
  3. Msauzi na mnaigeria ni kama kulwa na dotto hapo yanga imekula kwenu, sijui hawaangaliagi historia ya watu 😏

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic