October 10, 2021

 


MSHINDI mara 5 wa tuzo ya Ballon d'Or, mshambuliaji Criastiano Ronaldo ameweza kufikisha jumla ya mechi 200 katika Ligi Kuu England ambapo kwa sasa staa huyo anatumika ndani ya kikosi cha Manchester United.

Ikumbukwe kwamba mwaka 2020 tuzo hiyo haikuweza kutolewa kutokana na tatizo la janga la Corona ambalo liliweza kuvuruga mambo.

Kwa mwaka 2021 ipo kwenye mpango wa kutolewa na inatarajiwa kutolewa Novemba 29 mwaka huu na jina la staa huyo pia lipo kwenye orodha ya wale ambao wanawania tuzo hiyo kubwa.

Ronaldo ambaye aliibuka ndani ya Manchester United akitokea kikosi cha Juventus ameweza kuweka rekodi ya kufikisha mechi 200 jambo ambalo ni kubwa kwake kuweza kulifanya hivyo.

Rekodi zinaonyesha kwamba katika mechi hizo 200 ambazo amecheza ni mechi 160 aliweza kuanza kikosi cha kwanza na kuonyesha makeke yeke.

Pia katika mechi ambazo alianza kwa kufanyiwa mabadiliko ilikuwa ni mechi 40 na kufanya aweze kufikisha jumla ya mechi 200.

Katika mechi hizo ambazo amecheza ameweza kutupia mabao 87 huku akiweza kutengeneza jumla ya pasi 34 ambazo ziliweza kuleta mabao.

Mshikaji huyo ni mkali pia wa mipira iliyokufa ambapo kwa upande wa penalti amekuwa na zali la kufunga pia.

Ni mabao 11 aliweza kuyajaza kimiani kwa mipira iliyokufa lakini hii ilikuwa ni kwa penalti ambazo aliweza kuzipiga.

Msimu huu wa 2021/22 ameweza kufunga jumla ya mabao matano lakini sio kwenye ligi pekee bali ni kwenye michuano tofauti ambayo amecheza.

Pia ni mchezo mmoja aliweza kuanzia benchi kwa msimu huu ilikuwa kwenye mchezo wao dhidi ya Everton.

Jezi yake ambayo anaipenda kuivaa staa huyo ni namba 7 hata sasa akiwa ndani ya United anaivaa jezi hiyo ambayo ni pendwa kwake.

Amekuwa akivaa jezi namba 7 pia hata anapokuwa kwenye majukumu yake kwenye timu ya taifa ya Ureno.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic