Mashabiki kibao wa Simba sasa wamegeuza
jezi yenye jina la mshambuliaji wa Yanga, Saidi Bahanuzi kama kiburudisho kwao.
Bahanuzi alikosa penalty wakati Yanga
ilipopambana na Al Ahly, Jumapili iliyopita jijini Alexandria. Kama angefunga,
basi Yanga ingekuwa imefuzu.
Awali jezi hiyo ilianza kusambaa katika
mitanao mbalimbali ya kijaamii, lakini sasa mambo yamebadilika na inaanza
kuonekana mitaani.
Idadi ya wanaovaa jezi iliyoandikwa
Ahsante Bahanuzi imekuwa ikizidi kuonekana kwenye mitaa ya nini la Dar es
Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment