Kocha Msaidizi wa Yanga, Boniface
Mkwasa, amesema kikosi ni bora na kina uwezo wa kuifunga timu yoyote hapa
nyumbani kama maelekezo yakifuatwa kwa uhakika.
Lakini akasema mechi yao ya leo mjini
Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar itakuwa ngumu kutokana na kiwango duni cha
uwanja huo.
“Bado uwanja si mzuri sana, ndiyo maana
ninaweza kusema kutakuwa na ugumu katika mechi hiyo,” alisema Mkwasa.
“Utaona tofauti ya Yanga inapokuwa
inacheza kwenye uwanja duni na uwanja bora kama ule wa taifa, bado tuna
matatizo ya viwanja,” alisema Mkwasa.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara itakuwa ni
ya kwanza kwa Yanga tokea irejee nchini ikitokea Misri ilipokwenda kukipiga na
Al Ahly ambayo iliwang’oa mabingwa hao wa Tanzania Bara katika Ligi ya Mabingwa
Afrika.
0 COMMENTS:
Post a Comment