Mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe amesema sasa yuko fiti
kuendelea na kazi yake ya kupachika mabao.
Tambwe raia wa Burundi aliumia kichwani katika mechi dhidi
ya Prisons, Jumapili iliyopita.
“Niko vizuri kabisa, naweza kufanya mazoezi na ikiwezekana
nitacheza.
“Nataka kucheza mechi zote zilizobaki kama kocha atanipanga,
natamani pia kufunga tena,” alisema.
Tambwe ana mabao 19, akiwa amemfikia mfungaji bora wa misimu
miwili iliyopita, John Bocco wa Azam FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment