March 14, 2014


Mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe amesema sasa yuko fiti kuendelea na kazi yake ya kupachika mabao.

Tambwe raia wa Burundi aliumia kichwani katika mechi dhidi ya Prisons, Jumapili iliyopita.
“Niko vizuri kabisa, naweza kufanya mazoezi na ikiwezekana nitacheza.
“Nataka kucheza mechi zote zilizobaki kama kocha atanipanga, natamani pia kufunga tena,” alisema.
Tambwe ana mabao 19, akiwa amemfikia mfungaji bora wa misimu miwili iliyopita, John Bocco wa Azam FC.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic