July 28, 2014

KARIAKOO


Uongozi wa Yanga umekamilisha kila kitu kuhusiana na nyumba watakayoishi washambuliaji wake Jaja na Coutinho raia wa Brazil eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.


Jaja na Coutinho waliouomba uongozi wa Yanga waishi Kariakoo karibu na makao makuu ya klabu yao badala ya kupelekwa kwa ‘wanene’, Masaki au Oysterbay.
 
JAJA&COUTINHO WAKIWA MAZOEZINI NA KIKOSI CHA YANGA...
Habari za uhakika zinasema tayari Yanga imelipa nyumba hiyo na ilikuwa katika hatua za mwisho za ukarabati.

“Kuna mambo kadhaa ya kurekebisha ili wakae katika hali nzuri kabisa, ila masuala ya kodi yamekamilika,” kilieleza chanzo ambacho kinasimamia nyumba watakayoishi, kisha kikaendelea:

“Uongozi wa Yanga umekuja kumalizana nasi na sasa ni suala la wao kuingia tu, ila tuliwaomba kufanya ukarabati.”

Makocha Marcio Maximo na msaidizi wake, Leonaldo Leiva wao wataishi Masaki katika nyumba tofauti.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic