Kocha wa
timu ya vijana chini ya miaka 21 a Manchester City, Patrick Vieira amefanya
kitendo cha kijasiri baada ya kuamua kuvunja mechi kwa kuitoa timu yake nje.
LOGA AKIWA CROATIA. |
Vieira
alifanya hivyo kupinga vitendo vya ubaguzi wa rangi katika mechi ya kirafiki
kati ya timu yake dhidi ya NHK Rijeka ya Croatia ikiwa katika sehemu ya
kujiandaa na msimu mpya.
VIEIRA AKITOKA UWANJANI NA WACHEZAJI WAKE |
Croatia
ndiyo anakotokea Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic ambaye sasa yuko nchini
akiendelea kuinoa timu yake.
Kiungo
Seko Fofana raia wa Ufaransa ndiye aliyebaguliwa na mmoja wa wachezaji lakini
wenzake wakaonekana kumuunga mkono.
HUYU NDIYE ALIYEBAGULIWA |
Mara moja
Vieira ambaye ni nahodha wa zamani wa Arsenal aliamua kuingia uwanjani na
kuwatoa wachezaji wake.
Bosi wake,
Kocha Mkuu wa Man City, Manuel Pellegrini ameunga mkono kitendo hicho cha Vieira na kusema kama yeye
aliona sawa, basi oia anaona ni sahihi.
0 COMMENTS:
Post a Comment