October 12, 2021


 MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said Mohamed amesema kuwa kwa sasa mpango mkakati wao kama GSM ni kuhakikisha wanaimarisha kikosi cha Yanga ili kiwe imara kila idara kufanya vyema kwenye mashindano ya kimataifa msimu ujao.

Kwa sasa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi imeweka kambi Kigamboni katika kijiji cha Avic Town kwa ajili ya maandalizi ya mechi zijazo ndani ya ligi ambapo mchezo ujao itakuwa dhidi ya KMC, Uwanja wa Majimaji, Songea.

Kwa sasa imeelezwa kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga ambaye ni raia wa Burundi, Said Ntibanzonkiza ‘Saido’ kuna uwezekano kwenye dirisha dogo la usajili ataachwa na mabosi wake hao.

Tetesi hizo zinadai kwamba nafasi yake inatajwa kuchukuliwa na mshambuliaji tegemeo kwa sasa wa timu ya taifa ya Uganda ambaye anakipiga katika Klabu ya FC Ashdod ya Ligi Kuu Israel.

Nyota huyo anaitwa Fahad Bayo ambaye alizaliwa 10 mei 1998 katika mji wa Lugazi Uganda ana urefu wa 1.85.

10 COMMENTS:

  1. Bora yule Kazimoto wa Burundi wamuondoe maana ana dharau sana....

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mnato mwingi wakati ni majeruhi kila mara

      Delete
  2. Yaani mchezaji atoke Ligi Kuu ya Israel aje aichezee Yanga vs JKU ! Wakati mwingine muwe mnakuwa seriuos basi jamani!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ushaambiwa mbali na ligi kuu Tz lkn Yanga inajiandaa na mashindano ya kimataifa alf unashangaa??? Kuwa serious aisee

      Delete
    2. Kipi hakiwezekani! Mbona Banda alitoka sherrif akaja Simba?

      Delete
  3. Si subirini kipondo kingine, tulieni.

    ReplyDelete
  4. Yanga tupo gado,aje yeyote yule ni kichapo tu!

    ReplyDelete
  5. Yanga ndo imeanza mambo wengine tulieni tu mtaumia sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic