July 23, 2014



Kocha wa timu ya vijana chini ya miaka 21 a Manchester City, Patrick Vieira amefanya kitendo cha kijasiri baada ya kuamua kuvunja mechi kwa kuitoa timu yake nje.

LOGA AKIWA CROATIA.

Vieira alifanya hivyo kupinga vitendo vya ubaguzi wa rangi katika mechi ya kirafiki kati ya timu yake dhidi ya NHK Rijeka ya Croatia ikiwa katika sehemu ya kujiandaa na msimu mpya.


VIEIRA AKITOKA UWANJANI NA WACHEZAJI WAKE

Croatia ndiyo anakotokea Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic ambaye sasa yuko nchini akiendelea kuinoa timu yake.

Kiungo Seko Fofana raia wa Ufaransa ndiye aliyebaguliwa na mmoja wa wachezaji lakini wenzake wakaonekana kumuunga mkono.
HUYU NDIYE ALIYEBAGULIWA

Mara moja Vieira ambaye ni nahodha wa zamani wa Arsenal aliamua kuingia uwanjani na kuwatoa wachezaji wake.
Bosi wake, Kocha Mkuu wa Man City, Manuel Pellegrini  ameunga mkono kitendo hicho cha Vieira na kusema kama yeye aliona sawa, basi oia anaona ni sahihi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic