August 20, 2014



Na Makame Mohammed, Zanzibar
Kocha Mkuu mpya wa Simba, Mzambia, Patrick Phiri, ameshtushwa na taarifa za kipa wake, Juma Kaseja na beki wa kati Kelvin Yondani, kuichezea Yanga huku akitamka kuwa wataonana uwanjani.
Mzambia huyo alitua nchini wiki iliyopita kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho kinachojiandaa na Ligi Kuu Bara iliyopanga kuanza Septemba 20, mwaka huu huku akisaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuifundisha Simba.

Phiri alisema kuwa ni ngumu kuwazuia wachezaji kwenda kuichezea timu hiyo, yote ni katika kutafuta maisha.
Phiri alisema, kikubwa anawatakiwa kila la kheri wachezaji hao huku akiwataarifu wataonana uwanjani mara timu hizo zipokutana kwenye ligi na mashindano mengine.

“Ni maendeleo mchezaji anapotoka kwenda sehemu nyingine, lakini kwangu ninashangaa Kaseja na Yondani kwenda kuichezea timu pinzani.

“Ninaamini wachezaji hao wamefuata maslahi mazuri waliyoahidiwa Yanga katika kutafuta maisha, lakini kikubwa ninawatakia maisha mema huko walipo,” alisema Phiri aliyewahi kuwafundisha wachezaji hao wakiwa wanaichezea Simba.

SOURCE: CHAMPIONI JUMATANO

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic