August 20, 2014


KITENGE WAKATI AKIKABIDHIWA MKATABA MPYA WA E FM.


Mtangazaji mpya wa E FM Radio, Maulidi Kitenge anatarajia kuanza kusikika tena hewani kesho Alhamisi.

Kitenge maarufu kama jezi namba 10 mgongoni anatarajia kuanza kusikika katika kipindi kipya cha redio hiyo ambacho kitakuwa kikirushwa saa 1 usiku, kila siku.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Kitenge ambaye ni mtangazaji maarufu wa michezo nchini alisema wako katika maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kipindi hicho saa moja kamilini kesho Alhamisi.
“Maandalizi yanakwenda vizuri na Mungu akijaalia, Alhamisi tutaanza,” alisema Kitenge.

Kitenge na mtangazaji pacha wake, Katanga wamehamia E FM wakitokea Radio One.
Kitenge akifanya kazi Radio One kwa miaka 14 na siku nne zilizopita aliaga rasmi na kuanza makazi mapya na redio hiyo mpya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic