September 30, 2014

MWAKIBINGA (KUSHOTO) AKIWA NA BOSI MKUBWA WA AZAM TV, RHYS TORINGTON AMBAO NI KATI YA WADHAMINI WA LIGI KUU BARA.
Bodi ya Ligi Tanzania imetoa msimamo wake kuhusiana na lile sakata la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutaka lipewe fedha za udhamini za klabu kwa ajili ya shughuli zake lilizoziita ni za maendeleo ya soka.



TFF imeiagiza bodi ya ligi kukata kiasi cha asilimia tano tano kutoka kwenye udhamini wa Vodacom na Azam TV ili ipewe yenyewe.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga amesema wao ni wawakilishi wa klabu, hivyo wanabaki upande wa klabu.

"Bodi inazaliwa kutoka kwenye ubavu wa klabu, sisi ni wawakilishi wa klabu. Hivyo automatikale tunabaki upande wa klabu," alisema Mwakibinga.
Kama bodi hiyo itabaki upande wa klabu hizo 14, maana yake utakuwa umeziokoa kunyongwa fedha zao za udhamini.

Tayari klabu kupitia mwanasheria Dk Damas Ndumbaro zimepinga suala hilo na Mbeya City na Mtibwa Sugar zimetishia kwenda mahakamani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic