September 30, 2014

KIKOSI CHA YANGA KILICHOIFUNGA PRISONS MABAO 2-1.

Uongozi wa Yanga umewataka wanachama wake kusahau kuhusiana na suala la mchezo wa Prisons ya Mbeya na kutupia nguvu nyingi katika mechi ijayo dhidi ya JKT Ruvu.

Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu amesema kitu kizuri kwao kilikuwa kupata pointi tatu na sasa wanajipanga zaidi kwa ajili ya mechi ijayo.
NJOVU (KULIA) AKIWA NA BOSI WAKE, MWENYEKITI WA YANGA, YUSUF MEHBUB MANJI

"Kuangalia kilicho mbele yetu litakuwa jambo zuri sana, tumecheza dhidi ya Prisons na kushinda, hilo lilikuwa ni jambo zuri.
"Wako wanalalamika hatukucheza vizuri hasa kipindi cha pili, ni kweli lakini siku hazifanani na pia wajue wachezaji nao ni binadamu, kuna mtu anaamka vibaya na siku nyingine vizuri.
"Tushukuru tulipata pointi tatu na sasa tuna muda wa kujirekebisha na kufanya vema. Hakuna haja ya kufikiria mechi ya Prisons ilikuwaje," alisema Njovu.
Yanga ilianza Ligi Kuu Bara kwa kupoteza mechi ya kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar lakini wakazinduka mechi iliyofuata na kushinda mabao 2-1 dhidi ya Prisons lakini kipindi cha pili, timu yao haikucheza vizuri na kufanya Wajelajela kuutawala mchezo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic