September 21, 2014

MPIRA UMEKWISHA:

Dk 90, Kisiga anapiga mkwaju mwingine wa faulo, anaugonga Owino na kuwa goal kick.


DK 89, Kiongefa anakongana na kipa Shabani Kado, mshambuliaji huyo anatolewa nje na nafasi yake inachukuliwa na KIemba.

GOOOOOO...Dk 84, Rama Salim (yule blog hii iliyosema achungwe leo) anaifungia Coastal bao la kusawazisha mara baada ya kupiga faulo tamu ya mpira wa kufa.
Dk 76, Uhuru anapiga shuti ambalo linatoka nje, hata hivyo inaonekana liishaatokea.


Dk 74, Kiongera anapiga shuti kubwa linatoka nje ya langoDk 67, Yayo Lutimba anapiga shuti kali na kufunga ikiwa ni baada ya kupokea kasi ya Itubu.

Dk 64, Tambwe anatoka na nafasi yake inachukuliwa Paul Kiongera.
Dk 57, Yayo Lutimba anapiga shuti linatoka sentimeta chache la lango la Simba.


Dk 56, Rama Salim anapokea pasi nzuri lakini shuti lake linapanguliwa na Ivo na kuwa kona.
Dk 48, Okwi anaingia katika eneo la hatari kwa kasi lakini Tumba Sued anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira huo ambao ungeweza kuleta madhara.

HALF TIME:
Dk 38-44, Simba ndiyo wanatawala zaidi na kufanya mashambulizi, lakini si yale yenye madhara makubwa.


GOOOOOOO Dk 36, Simba inapata bao la pili kupitia Amissi Tambwe anayefunga kwa kichwa akiunganisha krosi safi ya Emmanuel Okwi aliyewazidi kasi mabeki wa Coastal.

Dk 25 Itubu Imbem anapiga shuti kali linalodakwa kiufundi na kipa Ivo Mapunda.
Dk 20, Okwi anampa pasi safi Chanongo ambaye anapiga krosi ambayo inakosa mtu.

Dk 12-16, timu zinashambuliana kwa zamu  huku mpira zaidi ukichezwa katika ya uwanja.


Dk 10, Chanongo anamtoka Sued lakini anawahi na kuokoa, inakuwa kona nyingine, lakini haina madhara.
GOOOOOOO....Dk 4, Kisiga anapiga bao kwa faulo baada ya Okwi kuwa ameangushwa na Tumba Sued.


Dk 4, Shabalala anapiga krosi nzuri, mabeki wa Coastal wanaokoa inakuwa kona, lakini isiyo na madhara.


Dk 1, Coastal Union wanapata kona ya kwanza inapigwa lakini inakuwa tasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic