October 25, 2014


Geilson Santana ‘Jaja’ ameamka baada ya kuifungia Yanga bao lake la kwanza kwenye Ligi Kuu Bara kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Stand United.

Lakini Jerry Tegete ndiye alikuwa kivutio baada ya kuingia kipindi cha pili na kupachika mabao mawili peke yake.
Tegete aliyeingia dakika ya 70 kuchukua nafasi ya Jaja, alifunga bao lake la kwanza katika dakika ya 77, likiwa la pili kwa Yanga, kabla ya kufunga la pili katika dakika ya 90.
Jaja alifunga bao lake mapema tu katika dakika ya 12 baada ya mpira kumkuta akiwa katika nafasi nzuri na kupiga fasta ukajaa wavuni.
Mechi hiyo kwenye Uwanja wa Kambarage ilikuwa nzuri huku Stand wakionyesha soka safi.
Hata hivyo Stand walikuwa na tatizo la umaliziaji kwani walishindwa kufunga kila walipoingia kwenye lango la Yanga.

Kuingia kwa Tegete na Hussein Javu kuliongeza kasi zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic