November 20, 2014

PHIRI AKIWASILI UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE LEO KWA AJILI YA SAFARI YA KUREJEA KWAO ZAMBIA.

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri ameondoka leo jijini Dar es Salaam kurejea kwao Zambia.

Phiri ameondoka na kusema anaamini atarejea kuinoa Simba.

Hata hivyo, safari yake ilionekana kuwa kama siri kutokana na baadhi ya viongozi kuwa waoga kuizungumzia.

Phiri amesema anakwenda likizo ya siku saba na anatarajia kurejea nchini mapema kuanza kambi na Simba kujiandaa na mechi ya bonanza kati yao dhidi ya Yanga.

"Naamini nitarudi, nakwenda nyumbani kwa likizo fupi halafu nitarudi kuendelea kupambana," alisema Phiri huku akitabasamu.

Kumekuwa na hofu kama kweli Phiri anaweza kurejea kutokana na kikosi chake kuonekana kutofanya vizuri katika mechi saba walizocheza huku wakishinda moja tu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic