November 20, 2014

DK NDUMBARO AKIWA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE, LEO.

Wakili maarufu nchini Dk Damas Daniel Ndumbaro ameendelea kufanya shughuli zake mbalimbali za kisheria huku akisubiri kusikilizwa kwa rufaa yake.

Dk Ndumbaro ameondoka leo jijini Dar es Salaam kwenda Arusha ambako kuna kongamano la wanasheria.

Amesema amekuwa akiendelea na shughuli zake za kisheria wakati akisubiri rufaa yake aliyokataa kwenye kamati ya rufaa ya TFF baada ya kufungiwa miaka saba.
TFF ilitangaza kumfungia kupitia kamati ya nidhamu, lakini rufaa yake aliyowasilisha haijasikilizwa, takribani mwezi sasa.

“Naendelea na shughuli za kisheria kama ambavyo vile nilizitetea klabu. Sasa nakwenda Arusha baada ya kumaliza shughuli nyingine kama hizi huko Kigali. Ndiyo maana mnaona kimya.

“Nikitulia nitarejea tena na kusisitiza suala la rufaa yangu, si kwamba nimekaa kimya tu,” alisema Dk Ndumbaro ambaye ni mwalimu wa sheria katika Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu Huria (Out).

sema  

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic