November 26, 2014


Uongozi wa timu ya Maafande wa Tanzania Prisons ya mkoani Mbeya, umesema unataka kusajili wachezaji watatu ili kuweza kukiongezea nguvu kikosi hicho.


Prisons ipo katika nafasi ya tatu kutoka chini kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi sita na inahitaji wachezaji watatu wenye uwezo na viwango vya hali ya juu ili kuweza kutoka hapo walipo.

Ofisa habari wa Prisons, Enock Mwanguku, alisema kuwa kikosi chao kina wachezaji wengi ambao bado hawajawatumia katika mikikimikiki ya ligi kuu, hivyo suala la kusajili halina umuhimu sana.


 “Kwa sasa hatuhitaji kufanya usajili kwa sababu timu yetu bado ina wachezaji wengi sana ambao tuliwasajili kipindi cha dirisha kubwa wakiwa bado wengine hawajacheza, lakini kama tukitaka kufanya usajili katika kikosi chetu, basi tutasajili wachezaji watatu ili kuongeza nguvu,” alisema Mwanguku.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic