December 19, 2014


Uongozi wa Simba chini ya Rais Evans Aveva umewarejesha baadhi ya wachezaji wake wa zamani kupitia kamati mbalimbali.

Aveva amesema waliorudishwa mpya ni pamoja na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Abdallah ‘King’ Kibadeni ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi pamoja na George Lucas ‘Gazza’ na winga machachari wa Simba enzi hizo, Dua Said ambao ni wajumbe katika kamati hiyo.

“Nimeunda kamati kwa ajili ya kuimarisha utendaji katika klabu yetu,” alisema Aveva.

Alizitaja kamati hizo pamoja na wenyeviti wake kuwa ni Kamati ya Ufundi, Mwenyekiti, Colin Frisch, Kamati ya Fedha, mwenyekiti, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, Kamati ya Soka la Vijana, mwenyekiti, Said Tully, Kamati ya Maadili, mwenyekiti, Samson Mbamba na katika Kamati ya Nidhamu, mwenyekiti ni Michael Ngallo.

Aidha, katika Kamati ya Uwekezaji na Masoko, mwenyekiti, Salim Abdallah huku mjumbe akiwa Azim Dewji, Kamati ya Mashindano, mwenyekiti, Mohamed Nassoro, huku Kamati ya Muda ya Matamasha, mwenyekiti, Gerlad Yambi na katika Kamati ya Wanachama na Matawi, mwenyekiti wake ni Kassim Dewji ambapo Kamati ya Usajili inaendelea kuwa chini ya Zacharia Hans Poppe.

Aveva aliongeza kuwa wanatarajia kuwa na mkutano mkuu Januari 11, mwakani katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbey, jijini Dar.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic