Uongozi wa Simba chini ya Rais Evans Aveva
umewarejesha baadhi ya wachezaji wake wa zamani kupitia kamati mbalimbali.
Aveva amesema waliorudishwa mpya ni pamoja na
aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Abdallah ‘King’ Kibadeni ambaye ni Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi pamoja na George Lucas ‘Gazza’ na winga
machachari wa Simba enzi hizo, Dua Said ambao ni wajumbe katika kamati hiyo.
“Nimeunda kamati kwa ajili ya kuimarisha
utendaji katika klabu yetu,” alisema Aveva.
Alizitaja kamati hizo pamoja na wenyeviti wake
kuwa ni Kamati ya Ufundi, Mwenyekiti, Colin Frisch, Kamati ya Fedha,
mwenyekiti, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, Kamati ya Soka la Vijana, mwenyekiti, Said
Tully, Kamati ya Maadili, mwenyekiti, Samson Mbamba na katika Kamati ya
Nidhamu, mwenyekiti ni Michael Ngallo.
Aidha, katika Kamati ya Uwekezaji na Masoko,
mwenyekiti, Salim Abdallah huku mjumbe akiwa Azim Dewji, Kamati ya Mashindano,
mwenyekiti, Mohamed Nassoro, huku Kamati ya Muda ya Matamasha, mwenyekiti,
Gerlad Yambi na katika Kamati ya Wanachama na Matawi, mwenyekiti wake ni Kassim
Dewji ambapo Kamati ya Usajili inaendelea kuwa chini ya Zacharia Hans Poppe.
Aveva aliongeza kuwa wanatarajia kuwa na
mkutano mkuu Januari 11, mwakani katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbey,
jijini Dar.
0 COMMENTS:
Post a Comment