January 31, 2015


Kutokana na vurugu zilizozuka katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza kati ya Majimaji na Friends Rangers, viongozi wa Friends Rangers wamedai kuwa wapo tayari kuiuza timu hiyo kutokana na kuchoshwa na tabia za wanasiasa na waamuzi kuvuruga michezo.


Mchezo huo uliopigwa juzi katika Uwanja wa Majimaji, Songea ulivunjika katika dakika ya 38 huku Majimaji ikiongoza kwa bao, ambapo bao la pili ndilo lililozua zogo kutokana na Friends kudai mchezaji wa Majimaji aliuweka mpira wavuni kwa mkono akiwa amelala chini wakati wa piga nikupige.

Kocha Msaidizi wa Friends, Herry Chibakasa ‘Mzozo’, ameliambia gazeti hili kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi ndiyo wanatakiwa kulaumiwa kwa kushindwa kuwepo mchezoni, hivyo ni bora waiuze tu timu yao.

“Inasikitisha sisi timu za walalahoi tunapigana lakini wachache ndiyo wanatuharibia, nasikitishwa na TFF au watu wa Bodi ya Ligi kutokuwepo katika mchezo huo wakati ulikuwa ni mchezo ambao unaamua nani apande daraja lakini wao wakapotezea.

“Kiukweli timu hii bora nitafute mteja tuuze kuliko kupoteza fedha nyingi kuendesha na kuchukua pesa za wananchi halafu wachache ndiyo wanakuja kuharibu, hii si nzuri kabisa, TFF wajipange jamani,” alisema Mzozo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic