Kutokana na vurugu zilizozuka katika mchezo wa Ligi
Daraja la Kwanza kati ya Majimaji na Friends Rangers, viongozi wa Friends
Rangers wamedai kuwa wapo tayari kuiuza timu hiyo kutokana na kuchoshwa na
tabia za wanasiasa na waamuzi kuvuruga michezo.
Mchezo huo uliopigwa juzi katika Uwanja wa
Majimaji, Songea ulivunjika katika dakika ya 38 huku Majimaji ikiongoza kwa
bao, ambapo bao la pili ndilo lililozua zogo kutokana na Friends kudai mchezaji
wa Majimaji aliuweka mpira wavuni kwa mkono akiwa amelala chini wakati wa piga
nikupige.
Kocha Msaidizi wa Friends, Herry Chibakasa ‘Mzozo’,
ameliambia gazeti hili kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi
ndiyo wanatakiwa kulaumiwa kwa kushindwa kuwepo mchezoni, hivyo ni bora waiuze
tu timu yao.
“Inasikitisha sisi timu za walalahoi tunapigana
lakini wachache ndiyo wanatuharibia, nasikitishwa na TFF au watu wa Bodi ya
Ligi kutokuwepo katika mchezo huo wakati ulikuwa ni mchezo ambao unaamua nani
apande daraja lakini wao wakapotezea.
“Kiukweli timu hii bora nitafute mteja tuuze
kuliko kupoteza fedha nyingi kuendesha na kuchukua pesa za wananchi halafu
wachache ndiyo wanakuja kuharibu, hii si nzuri kabisa, TFF wajipange jamani,”
alisema Mzozo.
0 COMMENTS:
Post a Comment