March 21, 2015






MPIRA UMEKWISHA:
MWAMUZI SIMON MBERWA ANAPULIZA FILIMBI YA MWISHO KATIKA DAKIKA 90.
Dk 90+3

Dk 87 Ally Nassor anapiga shuti kali lakini linapaa juu ya lango la Yanga
GOOOOOO Dk 83, Tambwe anaifungia Yanga bonge la bao kwa kichwa baada ya krosi ya Msuva
Dk 82, Msuva anapiga kichwa tena lakini kinakuwa lakini kwa kipa wa Mgambo.


Dk 78, anatolewa Sherman anaingia Hussein Javu
GOOOOOOOO Dk 77, Msuva anaifungia Yanga bao baada ya purukushani katika lango la Mgambo.

Dk 75, krosi safi ya Joshua, mpira unatua kichwani mwa Tambwe lakini kipa wake anakuwa fundi na kudaka.

Dk 69, shuti kali la Niyonzima linaokolewa na kipa wa Mgambo na kuwa kona isiyo na matunda.


Dk 67, Yanga wanafanya mashambulizi mfululizo lakini Mgambo wanaokoa tena.


Dk 66 krosi nzuri ya Niyonzima, mabeki Mgambo wanaokoa na kuwa kona.
Dk 60 Msuva anaiwahi vizuri krosi ya Juma Abdul na kupiga vizuri lakini inagonga mwamba na kutoka nje.
Dk 57 Salim anapiga shuti kali lakini mpira unawababatiza mabeki wa Yanga

Dk 53, Sherman anajaribu shuti kali lakini linapaa juu.




Dk 50, Msuva analambwa kadi ya njano kutokana na kucheza faulo ya makusudi. Halikadhalika Salim Mlima wa Mgambo naye anapigwa kadi ya njano.
Dk 47, Fullyzully Maganga analambwa kadi ya njano kwa kujiangusha.


Dk 46 Tambwe anapiga shuti linagonga mwamba.
MAPUMZIKO:
Dk 45 Msuva anapata pasi nyingine safi kutoka kwa Niyonzima. Lakini anapiga shuti ‘mtoto’

Dk 42, Msuva anapata nafasi nyingine nzuri baada ya pasi ya Sherman lakini anashindwa kufunga. Kocha Hans anasimama na kuanza kufoka.

Dk 40, Said Juma Makapu analambwa kadi ya njano kwa faulo mbaya.
Dk 36 Gilla anapiga krosi safi katika lango la Yanga, inaokolewa na kuwa kona.


Dk 32, Msuva anapata nafasi nzuri lakini akiwa amebaki na kipa anabutua juuu.
Mechi imeanza kwa kasi licha ya uwanja kuwa umeloa tope.


Yanga ndiyo wanaonekana kuwa vizuri zaidi kutokana na kupeleka mashambulizi mengi zaidi.

Iwapo Yanga watatulia, basi wanawza kupata bao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic