April 21, 2015

Dk 4 ZA NYONGEZA
Dk 90, Chanongo anapata nafasi nzuri akimtazama Dida, anashindwa kufunga na kupiga nje
Dk 90, Ngassa anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Danny Mrwanda

Dk 85&89 Yanga na Stand mpira unaonekana kuchezwa katikati zaidi. Yanga wanapunguza mashambulizi wakionekana kuridhika na matokeo
KADI Dk 84 Tambwe analambwa kadi ya njano kwa kucheza kibabe

Dk 79, Javu anawachambua mabeki watatu wa Stand, lakini anaangushwa na mpira unaokolewa
GOOOOOOO Dk 79 Msuva anafunga vizuri mkwaju wa penalti, Yanga tatu

PENAAAAT Dk 77 Tambwe anaangushwa na mwamuzi anaamuru ipigwe penalti...
Dk 72,  Ngassa anapoteza nafasi nyingine nzuri baada ya kupewa pasi na Msuva, anapaishaaaa

Dk 64 Elly anafunga bao safi kwa shuti kali baada ya kupokea pasi nzuri ya Chidiebere....
KADI Dk 63 Chanongo analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Ngassa
Dk 56, Chiedebere anapiga kichwa safi ndani ya eneo la hatari lakini mpira unapaa kidogo tu

Dk 48&50 wanafanya mashambulizi matatu, wanapata kona mbili na zote wanashindwa kuzitumia kufunga
Dk 46, Dida anafanya kazi ya ziada baada ya baada ya Stand kufanya shambulizi langoni mwa Yanga
Dk 46, Yanga wanamtoa Coutinho na nafasi yake inachukuliwa na Kpah Sherman

MAPUMZIKO
Dk 45+4 
Dk 45, Tambwe anapiga kichwa kikali kama shuti lakini kipa Stand anadaka kwa ustadi mkubwa

Dk 45, Ngassa anaifungia Yanga bao la pili baada ya kugongeana vizuri na Juma Abdul aliyetokea wingi ya kulia kupanda kusaidia mashambulizi

Dk 45, Chiedebere anaingia kwenye eneo la hatari akijaribu kuwapita Twitte na Makapu, wanaokoa na kuwa kona isiyo na faida
Dk 43, Stand wanaonekana kukaa nyuma kwa wingi wakilinda zaidi na kushambulia kwa kushitukiza
Dk 41, Juma Abdul anapiga krosi safi kabisa lakini Msuva anashindwa kuunganisha vizuri na inakuwa goal kick


Dkk 37, Elly anapata nafasi nyingine lakini anashindwa kuwa makini na kupaisha mpira juu
Dk 33, krosi safi ya Msuva lakini kipa anawahi kuruka na kudaka kichwani mwa Tambwe

GOOOOO Dk 30 Tambwe anaifungia Yanga baada ya kuiwahi krosi ya Ngassa na kufunga kwa ulaini 
Dk 28 Ngassa anapiga shuti kali lakini linaokolewa na kuwa kona isiyozaa matunda

GOOOOOO Dk 20, Elly Khalifa anafungia Stand bao la kwanza baada ya Twitte kufanya kosa kwa kuruka juu na kuukosa mpira, ukamfikia mfungaji naye kufunga bao safi kabisa.


Dk 17 pasi nzuri ya kisogo ya Amissi Tambwe inamfikia Coutinho, anapiga shuti kali sana lakini kipa anaokoa na kuwa kona isiyo na matunda.


Dk 12 Ngassa anashindwa kufunga akiwa katika eneo la 18 na kipa anaudaka kwa ulaiinii
Dk 9 mechi inaanza kuchangamka kwa kila timu kujipanga na kushambulia

Dk 8, Stand wanafanya shambulizi la kwanza lakini Chiedebere anawahi kutoka na kuwa ameotea
Dk 4, Yanga wanagongeana vizuri na kutengeneza nafasi nzuri ya kwanza, mpira unamfikia Coutinho anapiga shuti la chinichini lakini anashindwa kulenga lango.
Mechi imeanza na timu zinaonyesha kusomana 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic