April 1, 2015



Wachezaji wa Yanga wametakiwa kujituma zaidi kwa kuwa mambo bado hayajakaa kama anavyotaka kocha wao Hans van der Pluijm.


Pluijm raia wa Uholanzi amesema anaamini wachezaji wa Yanga wanaweza kufanya vizuri zaidi ya wanavyofanya sasa.

“Lakini haiwezi kuwa lahisi kama watajisahau. Hivyo nimekuwa nikiwasisitiza kujituma kila mara.

“Mafanikio yakipatikana wengi hujisahau mapema, mimi naona wachezaji wanaweza kufanya vizuri zaidi ya hapa.

“Kikosi changu ni bora lakini bado naamini kina ubora zaidi. Hatuwezi kufanikiwa bila ya kujituma.

“Najua kujifunza ni kufanya mambo tena, tena na tena bila ya kuchoka na ndiyo tumekuwa tukiendelea kufanya hivyo,” alisema Pluijm.

Kocha huyo pia amesisitiza suala la mechi yao ya marudiano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya FC Plutnum kwamba ni muhimu zaidi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic