Beki wa zamani wa Simba,
Talib Hilal na kikosi chake cha timu ya taifa ya ufukweni ya Omani, wametoa
zawadi ya ubingwa wa Asia kwa Mfalme wa Qaboos wa Oman.
Talib aliyewahi kuichezea
na kuifundisha Simba hadi kuipa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mwaka 2008, wametoa
ubingwa huo kwa Mfalme wao.
Oman wamefanikiwa kuwa
mabingwa kwa kuwafunga Japan katika michuano ya Asia ya Ufukweni iliyofanyika
jijini Doha Qatar.
Pamoja na ubingwa huo,
Talib ameiongoza Oman kupata nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia la Ufukweni
litakalofanyika nchini Ureno.
Uamuzi wa kutoa ushindi huo
kama zawadi kwa Mfalme Qaboos umetokana na namna yeye na serikali yake kujali
michezo kwa kiasi kikubwa ukiwemo mchezo huo wa soka la ufukweni.
0 COMMENTS:
Post a Comment