April 1, 2015

AVEVA (KUSHOTO) AKIWA NA BOSI WA EAG GROUP, IMANI KAJURA 

Kampuni ya EAG Group Limited, imeingia mkataba wa miaka mitano na klabu Simba kwa ajili ya kuitafutia mipango thabiti ya kuiendesha timu hiyo kuhakikisha inapiga hatua katika maendeleo yake.


EAG Group iliingia mkataba na timu hiyo leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun iliyopo Posta jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Rais wa Simba, Evans Aveva alisema kuwa kwa kumpitia udhamini wa kampuni hiyo wameandaa tuzo mbalimbali kwa wachezaji wao kuhakikisha wanajituma uwanjani.

Aveva alizitaja tuzo hizo ni ya mchezaji bora wa mwaka atakayepewa gari jipya, mchezaji kijana mwenye kipaji atkayepewa milioni 5 na mchezaji mwenye nidhamu atakayeramba milioni moja.

Pia, wachezaji hao wote kila mmoja atapewa zawadi ya simu aina ya Huawei yenye thamani ya shilingi milioni moja ambao nao wameingia kwenye udhamini huo.

“Lengo tunataka kuona timu yetu inapiga hatua katika soka ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika Mashariki na Kati na ndiyo tumetoa zawadi hizo kwa ajili ya kuwapa morali wachezaji wetu kupitia Kampuni ya EAG Group Limited na Huawei,” alisema Aveva.


Pia Mkurugenzi wa kampuni ya EAG Group, Imani Kajula alisema kuwa, huo ndiyo wa udhamini kwao, wamepanga kuleta mabadiliko ya soka kwa kuhakikisha wanawekeza zaidi kwa vijana kwa kuanza na Simba.

2 COMMENTS:

  1. Simba haina viongozi ....watu wajanja wajanja...unaweza vipi kushindwa kutimiza mahitaji ya mchezaji kessy...halafu mnaforce ushindi ubwege

    ReplyDelete
  2. Hizo ni campaign ambazo hazina msingi!! Hauwezi timiza ata ahadi za malipo, halafu unawaza kutoa zawadi ya gari!!:Acheni kuwsongopea vijana watoroke kwenye vilabu vyao kwa ajili ya ujinga wa vilabu vinajiita vikongwe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic