April 20, 2015


Yanga imepanga kushinda mechi zake tatu zijazo za Ligi Kuu Bara ili iwe bingwa kabla ya kwenda nchini Tunisia kupambana na Etoile du Sahel.


Mkuu wa kitengo cha habari cha Yanga, Jerry Muro amesema wanataka kupambana washinde mechi tatu.
“Lengo ni kushinda tatu zote, ili tukienda kupambana na Etoile tayari tunakuwa mabingwa,” alisema Muro.

“Tunajiandaa ili tushinde mechi ya kesho dhidi ya Stand United. Baada ya hapo, ni zamu ya anayefuatia,” alijigamba Muro.

Yanga itapambana na Etoile wiki mbili zijazo kuwania kusonga mbele katika Kombe la Shirikisho.
Tayari kuna ugumu baada ya Yanga kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Waarabu hao jijini Dar. Lakini wachezaji wameahidi kupambana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic