April 20, 2015


Kocha wa makipa wa timu za taifa za Oman na mkufunzi anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Haroon Amur Al Siyabi ameendelea kuwanoa makipa wa Simba, leo.

Al Siyabi ameendelea na mazoezi kuwanoa makipa hao kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Makipa hao akiwemo Ivo Mapunda, wamekuwa wakifundishwa mbinu mbalimbali za kisasa za ulinzi kwa makipa.
Al Siyabi alikuwa akiwaonyesha mambo kadhaa ya namna ya kudaka, kuwasoma washambuliaji na nini cha kufanya ili kujilinda zaidi.
Kocha huyo nguli katika kazi hiyo ya kunoa makipa, pia amewahi kumnoa kipa wa zamani wa Simba, Juma Kaseja.

Hata hivyo imeelezwa Al Siyabi anatarajia kuondoka nchini siku mbili sijazo kurejea kwao Oman kuendelea na majukumu mengine.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic