April 21, 2015


Suala la mrembo anayedaiwa kuwa mpenzi wa kipa Peter Manyika limeendelea kutajwa kuwa ndiyo sababu ya kushuka kwa kiwango chake.


Kocha wa Simba, Goran Kopunovic amemteremsha Manyika kucheza kikosi cha pili ili kuinua kiwango chake.
Lakini taarifa za ndani kutoka Simba zimeeleza mrembo huyo aitwaye Naima maarufu kama Nimaa ndiyo chanzo cha kuporomoka kwa kiwango.
“Hivi karibuni alisema asifuatwefuatwe, Manyika anaona kama anaonewa watu kumueleza kuhusu huyo mpenzi wake.

“Lakini kocha analalamika kuwa ameonyesha kiwango cha chini katika mechi zilizopota. Lakini yeye ni mbishi sana,” kilieleza chanzo.
Mara ya kwanza baada ya kunaswa na mrembo huyo, Manyika alikanusha na kudai Nimaa ni rafiki yake tu.


Lakini kwa sasa hali ilivyo, wawili hao wamekuwa wakijiachia hadharani na kuachana na mambo ya woga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic